Watu 37 wafariki na wengine zaidi ya 200 kujeruhiwa katika ajali ya moto nchini Bangladesh
2022-06-06 08:47:19| CRI

Mkuu wa Wilaya ya Chattogram nchini Bangladesh Mohammad Mominur Rahman amethibitisha kuwa, watu 37 wamefariki na wengine zaidi ya 200 kujeruhiwa katika ajali ya moto iliyotokea Jumapili kwenye bohari ya makontena, kilomita 242 kusini mashariki mwa mji mkuu wa nchi hiyo, Dhaka.  

Ajali hii ilitokea katika moja ya kontena lililokuwa limehifadhi vitu vya kemikali katika uwanja wa makontena uliopo Sitakunda, kitongoji cha mji wa Chattogram.

Waathiriwa wote wamepelekwa hospitalini, wengi wakiwa na majeraha madogo au makubwa, huku baadhi yao wakiwa katika hali mbaya, na ofisa wa zima moto ameonya kuwa idadi ya vifo inaweza kuongezeka.

Mkuu wa wilaya hiyo amesema, vitengo 16 vya zima moto vimejitahidi kuzima moto huo, na moto huo umedhibitiwa.