Rais wa China atoa wito wa juhudi za kutafuta masikilizano kati ya binadamu na mazingira
2022-06-07 09:08:32| CRI

Rais Xi Jinping wa China amesema mazingira ya asili ni msingi wa uhai wa binadamu na maendeleo, na  kulinda mazingira mazuri ya kiikolojia ni dhamira ya nchi zote duniani.

Rais Xi amesema hayo katika maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani iliyosherehekewa Jumapili iliyopita. Amesema tangu Mkutano mkuu wa 18 wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China  uliofanyika mwaka 2012, nchi hiyo imeweka ulinzi wa ikolojia kuwe pendekezo muhimu katika kutimiza maendeleo ya nchi hiyo.

Rais Xi amesisitiza kuwa, Chama cha Kikomunisti cha China na nchi nzima vinapaswa kudumisha malengo ya kimkakati katika kuimarisha ulinzi wa ikolojia, mabadiliko ya kijani katika maeneo yote ya maendeleo ya jamii na uchumi, kuratibu juhudi za kukabiliana na uchafuzi, kulinda mifumo ya ikolojia na kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi. Pia kufanya kazi kwa bidii ili kujenga China nzuri ambayo watu na mazingira wanaishi kwa masikilizano, ili kuendelea kutoa mchango zaidi katika kujenga dunia nzuri na safi.