China yapinga ripoti iliyotolewa na Marekani kuhusu uhuru wa kuabudu duniani
2022-06-07 09:00:43| cri


 

Msemaji wa Wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Zhao Zhijian jana amesema China inapinga vikali ripoti iliyotolewa na Marekani kuhusu uhuru wa kuabudu duniani.

Amesema mambo yanayohusu China kwenye ripoti hiyo na hotuba ya waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken kuhusu sera kwa China hayakuzingatia ukweli, yamejaa ubaguzi wa kiitikadi, kukashifu sera ya dini ya China, na kuingilia kati mambo ya ndani ya China.

Bw. Zhao amesema kuheshimu na kulinda uhuru wa kuabudu ni sera ya kimsingi ya Chama cha Kikomunisti cha China na serikali ya China.