Idadi ya watu waliofariki kutokana na kuporomoka kwa jengo nchini Iran yafikia 41
2022-06-07 09:03:27| CRI

Idadi ya watu waliofariki katika jengo lililoporomoka tarehe 23 mwezi uliopita katika mji wa Abadan kusini magharibi mwa Iran imeongezeka hadi 41 baada ya maiti tatu kupatikana kutoka kwenye kifusi.

Naibu mkuu wa Mkoa wa Khuzestan, Ehsan Abbaspour amesema maiti zilizopatikana zimetambuliwa, na kazi ya uokoaji itaendelea hadi mwathirika wa mwisho atakapopatikana kutoka kwenye vifusi.

Shirika la habari la Iran la Mizan limeripoti kuwa, watu 10 walikamatwa kutokana na tukio hilo, akiwemo mkuu wa mji wa Abadan.