Nchi za BRICS zaimarisha ushirikiano wa fedha
2022-06-07 09:10:09| CRI

Mkutano wa Pili wa Mawaziri wa nchi za BRICS na wakuu wa Benki Kuu wa mwaka 2022 umefanyika Jumatatu kwa njia ya mtandao.

Mkutano huo umefikia makubaliano kuhusu matokeo ya ushirikiano wa fedha kati ya nchi za BRICS yaliyopatikana mwaka huu, na kupitisha Taarifa ya pamoja ya mawaziri wa fedha wa nchi hizo na wakuu wa Benki Kuu.

Taarifa hiyo ya pamoja inafuatilia matishio ya uchumi na fedha yanayoikabili dunia, na kusisitiza kuwa mfumo wa fedha duniani unatakiwa kuhudumia maslahi ya nchi zote, pia inapongeza kuharakishwa kwa mchakato wa utekelezaji wa Ajenda ya Maendeleo Endelevu ya Umoja wa Mataifa ya Mwaka 2030, ili kuhimiza maendeleo ya dunia yawe na nguvu zaidi, ya kijani na mazuri.

Waziri wa Fedha wa China Liu Kun amesisitiza kuwa nchi za BRICS zinatakiwa kuimarisha mshikamano na ushirikiano, kukuza mawasiliano na uratibu, na kulinda kwa pamoja afya ya binadamu, na kuhimiza kufufuka kwa uchumi duniani kwa hatua madhubuti, kulinda kwa pamoja uendeshaji wenye utulivu wa mfumo wa kimataifa wa uchumi na fedha, na kuhimiza mchakato wa kukamilisha kanuni na mfumo wa usimamizi wa uchumi duniani.