Ethiopia ina matarajio ya ushirikiano mzuri na China kwenye sekta ya mazingira
2022-06-07 09:06:29| CRI

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Mazingira nchini Ethiopia Getahun Garedew amesema, nchi hiyo na China zinaweza kuimarisha ushirikiano kwenye sekta ya mazingira na kutimiza maendeleo yasiyosababisha uharibifu wa mazingira.

 Akizungumza na Shirika la Habari la China Xinhua hivi karibuni, Bw. Garedew amesema Ethiopia iko tayari kuboresha ushirikiano na China ili kuiga mafanikio ya nchi hiyo katika ulinzi wa mazingira. Amesema uhusiano kwenye sekta ya mazingira unahusisha uhamishaji wa teknolojia, kubadilishana uzoefu na kuhakikisha uwekezaji unakuwa rafiki kwa mazingira.

 Wakati huohuo, Bw. Garedew amezipongeza kampuni za China zilizowekeza nchini Ethiopia kutokana na umakini wake katika kuzingatia  ulinzi wa mazingira, na kusisitiza kuwa Ethiopia imejitolea kikamilifu katika ulinzi wa mazingira, jambo linaloendana na malengo ya maendeleo ya uchumi na jamii nchini humo.