“Kuthubutu kufanya jua na mwezi kung'aa katika anga mpya”, huu ni msemo wa Mao Zedong, “Mambo yote katika maisha yanapaswa kufanywa na sisi wenyewe” na “Ni nani anayethubutu kusema kwamba vizazi vichanga vilivyo na uwezo mkubwa haviwezi kuwazidi wazee?” ni miongoni mwa misemo mitano iliyonukuliwa na rais Xi Jinping katika maadhimisho ya miaka 100 ya kuzaliwa kwa Umoja wa Vijana wa Chama cha Kikomunisti cha China CPC.