Watu wenye matatizo ya kimaisha kutokana na janga la COVID-19 kupata pesa za misaada
2022-06-08 09:36:19| cri


 

Wizara ya mambo ya kiraia na Wizara ya fedha ya China zimetoa taarifa ya pamoja zikitaka serikali za mitaa kuhakikisha maisha ya kimsingi ya raia wenye matatizo ya kimaisha, ili kukabiliana na athari zilizoletwa na janga la COVID-19 kwa maisha yao.

Taarifa hiyo imesema, sehemu zilizoathiriwa zaidi na janga hilo zinaweza kuwasaidia kifedha kwa muda raia wenye matatizo ya kiuchumi.

Taarifa hiyo pia imezitaka serikali mbalimbali za mitaa zifuatilie hali ya mabadiliko ya bei za bidhaa, na kuzindua kwa wakati utaratibu wa kuunganisha vigezo vya misaada na uhakikishaji wa kijamii na ongezeko la bei za bidhaa, na kulipa ruzuku ya bei ya muda kwa wakati na kwa ukamilifu.