Rais wa Uganda asema Afrika inafanya mazungumzo na wahusika wa kimataifa kuhusu mgogoro wa Ukraine
2022-06-08 08:44:17| CRI

Rais Yoweri Museveni wa Uganda amesema viongozi wa Afrika wanafanya mazungumzo na wahusika wa kimataifa kuhusu mgogoro wa Ukraine, ikiwa ni juhudi za kukabiliana na bei kubwa ya bidhaa.

Akitoa hotuba ya Hali ya Taifa katika bunge la nchi hiyo, rais Museveni amesema bei kubwa ya bidhaa katika bara la Afrika inatokana kwa kiasi kikubwa na mgogoro wa Ukraine na vikwazo dhidi ya Russia.

Amesema njia mbadala ya kukwepa bei kubwa ya kuagiza bidhaa kutoka nje ni kujikita zaidi kwenye bidhaa za ndani, kama vile unga wa muhogo na ndizi na mafuta ya alizeti na soya kwa ajili ya mapishi.

Amesisitiza kuwa, serikali yake haitapunguza kodi ili kukabiliana na bei kubwa ya bidhaa.