Watu 17 wamefariki katika ajali ya treni ya abiria jana nchini Iran.
Shirika la Reli la Iran limesema, treni iliyokuwa na abiria 430 iligongana na mashine ya kuchimba na kuacha njia na kusababisha uharibifu wa mabehewa sita. Kazi ya uokoaji bado inaendelea.