Siku ya Mtoto wa Afrika--Malezi na Makuzi ya watoto wa Afrika kutokana na janga la COVID-19
2022-06-10 09:53:17| CRI

Siku ya Mtoto wa Afrika ni siku inayosherehekewa kila mwaka tarehe 16 Juni tangu mwaka 1991 ilipoteuliwa na Umoja wa Afrika katika kuenzi michango ya watoto walioshiriki katika maandamano katika mji wa Soweto, Afrika Kusini mwaka 1976 pamoja na kujengea jamii uelewa juu ya umuhimu wa elimu bora kwa watoto.

Katika siku hiyo ya kila mwaka, mataifa, jumuia mbalimbali na jumuia za kimataifa pamoja na wadau mbalimbali hukusanyika pamoja kwa ajili ya kujadili fursa na changamoto zinazowakumba watoto katika bara la Afrika. Katika miaka ya hivi karibuni, binadamu inakumbwa na janga la COVID-19, na watoto ndio wanaoathiriwa zaidi katika janga hili. Katika kipindi cha leo cha Ukumbi wa Wanawake tutaangazia suala la Malezi na makuzi ya watoto wa Afrika hususan kutokana na janga la COVID-19.