Waziri Mkuu wa Palestina atoa mwito wa kuanzisha ushirikiano wa kimataifa kukomesha ukaliaji wa Israel
2022-06-13 08:39:51| CRI

Waziri mkuu wa Palestina Bw Mohammed Ishtaye ametoa mwito wa kuanzishwa kwa ushirikiano wa kimataifa ili kuishinikiza Israel kukomesha ukaliaji wake kwenye maeneo ya Palestina na kulinda suluhisho la nchi mbili.

Bw. Ishtaye ametoa mwito huo katika mji wa Ramallah wakati akikutana na Maya Tissafi, naibu waziri wa mambo ya nje wa Uswisi na mkuu wa idara ya Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini.

Bw. Ishtaye ameitaka Uswisi na Jumuiya ya kimataifa kuishinikiza Isarel kufuata na kuheshimu makubaliano ya amani yaliyosainiwa na kuacha hatua zote za kukiuka mamlaka ya Palestina.

Bw. Ishtaye pia alisema kwenye mahojiano na televisheni ya Palestina, kuwa leo Umoja wa Ulaya utapiga kura kuhusu Umoja huowa Ulaya kuanza kutoa tena msaada kwa Palestina.