Mkutano wa 12 wa mawaziri wa WTO wafunguliwa huko Geneva
2022-06-13 08:53:29| CRI

Mkutano wa 12 wa mawaziri wa Shirika la Biashara Duniani WTO umefunguliwa katika makao makuu ya shirika hilo huko Geneva, Uswisi.

Katika mkutano huo wa siku nne, wanachama wa shirika hilo watajadili masuala mbalimbali ikiwa ni pamoja na kusamehe hakimiliki ya ujuzi kuhusu msamaha wa hakimliki za chanjo zinazohusiana na biashara (TRIPS), mwitikio wa janga, ruzuku ya uvuvi, kilimo, usalama wa chakula pamoja na mageuzi ya WTO na vipaumbele vyake vya kazi katika siku za baadaye.

Mkurugenzi mkuu mtendaji wa shirika hilo Bibi Ngozi Okonjo-Iweala, amesema hivi sasa dunia inakabiliwa na misukosuko mbalimbali ikiwemo janga la Corona, ukosefu wa chakula, mabadiliko ya tabianchi na migogoro ya kikanda, huku akitoa wito kwa pande zote kufanya juhudi za pamoja kutatua matatizo hayo.

Amesema hakuna nchi moja inayoweza kutatua misukosuko hiyo peke yake, na sasa ndio wakati wa dunia nzima kufanya juhudi kwa pamoja.