Rais Xi alipongeza gazeti la Ta Kung Pao kwa kuadhimisha miaka 120
2022-06-13 08:28:01| CRI

Rais Xi Jinping wa China jana jumapili alitoa barua ya pongezi kwa gazeti la Ta Kung Pao, ambalo ni moja ya magazeti makongwe ya lugha ya kichina yenye makao makuu mkoani Hongkong kwa kuadhimisha miaka 120 tangu kuanzishwa kwake.

Kwenye barua hiyo, Rais Xi amelihimiza gazeti hilo kuendeleza desturi ya uzalendo, kutafuta maendeleo ya kivumbuzi na kutoa ripoti nyingi zaidi nzuri kuhusu utekelezaji tulivu na endelevu wa mfumo wa “Nchi Moja, Mifumo Miwili”.

Rais Xi ametoa wito kwa gazeti la Ta Kung Pao kuendelea kuinua ushawishi wake, na kuchangia zaidi kwenye utimizaji wa Ndoto ya Taifa la China ya Kutimiza Ustawi Mpya.