Idadi ya wakenya wanaokabiliwa na njaa kutokana na ukame yaongezeka hadi milioni 4.1
2022-06-14 08:33:26| CRI

Mamlaka ya kitaifa ya kukabiliana na ukame nchini Kenya NDMA imesema idadi ya watu wanaokabiliwa na baa la njaa kutokana na ukame nchini humo imeongezeka hadi kufikia milioni 4.1 katika mwezi Juni kutoka milioni 3.5 ya mwezi Mei.

Kwa mujibu wa Ripoti ya tathmani iliyotolewa Jumatatu na mamlaka hiyo, hali ya ukame nchini humo imeendelea kuzorota, na asilimia kubwa ya watu walioathirika wako kwenye maeneo 19 kati ya maeneo yote 23 kame au yaliyo nusu kame, janga ambalo linatokana na ukosefu wa mvua katika mwaka 2021 na kumalizika mapema kwa msimu wa mvua wa mwaka huu.