Rais wa Rwanda amtunuku tuzo ya heshima katibu mkuu wa Shirika la Mawasiliano la kimataifa ITU
2022-06-15 08:41:49| CRI

Rais Paul Kagame wa Rwanda amemtunuku katibu mkuu wa Shirika la Mawasiliano la kimataifa ITU Bw. Zhao Houlin nishani ya heshimu ya Rwanda (Agaciro), kwenye hafla iliyofanyika katika ofisi ya rais mjini Kigali.

Tuzo ya Agaciro yenye maana ya heshima, hutolewa kwa wakuu wa nchi, wakuu wa mashirika ya kimataifa, na maofisa wa ngazi ya juu waliotoa mchango mkubwa kwenye kuendeleza mambo mazuri nchini Rwanda na nje ya Rwanda.

Tuzo hiyo imetolewa wakati Rwanda inakuwa nchi ya kwanza ya Afrika kuwa mwenyeji wa mkutano wa Shirika la Mawasiliano la kimataifa ITU, unaofanyika kuanzia Juni 6 hadi 16.

Bw. Zhao ambaye ni raia wa China aliteuliwa kuchukua nafasi hiyo mwaka 2014, na aliteuliwa tena mwaka 2018 kuendelea na nafasi hiyo.