China yaisaidia Tanzania kuhimiza elimu ya ufundi kazi kupitia mradi wa pamoja
2022-06-17 08:41:57| CRI

Tanzania na China zimezindua mradi wa pamoja wenye lengo la kuhimiza elimu ya ufundi kazi kupitia vigezo vipya vya elimu hiyo nchini Tanzania.

Mradi wa mapitio na maendeleo ya vigezo vya ufundi kazi uliozinduliwa jumatano, unafadhiliwa na Shirikisho la elimu ya ufundi kazi la China na Tanzania, na kusimamiwa na baraza la taifa la elimu ya ufundi kazi, teknolojia na mafunzo la Tanzania (NACTVET).

Akiongea kwenye uzinduzi huo, ofisa wa Shirikisho la elimu ya ufundi kazi la China na Tanzania Bw. Jiang Yilin, amesema kupitia mradi huo jumla ya vyuo 43 vya ufundi kazi vya China vitashiriki kwenye awamu ya kwanza, itakayohusisha vigezo 54 tofauti vya ufundi kazi.

Katibu mkuu wa baraza la taifa la elimu ya ufundi kazi, teknolojia na mafunzo la Tanzania Bw. Adolf Rutayuga amesema mradi huo utahimiza maendeleo ya elimu ya ufundi kazi na mafunzo nchini Tanzania na kuweka msingi wa vigezo vipya vya elimu.