Rais wa China ahudhuria mkutano wa 25 wa Baraza la Kimataifa la Uchumi la St. Petersburg
2022-06-19 15:05:30| CRI

Rais Xi Jinping wa China amehudhuria na kuhutubia mkutano wa 25 wa Baraza la Kimataifa la Uchumi la St. Petersburg uliofanyika kwa njia ya video.

Rais Xi amesema, hivi sasa kutokana na mabadiliko makubwa ya dunia na janga la COVID-19, uchumi wa dunia umekabiliwa na changamoto kubwa, huku utekelezaji wa malengo ya maendeleo endelevu ya mwaka 2030 ya Umoja wa Mataifa pia ukikabiliwa na changamoto nyingi ambazo hazijawahi kushuhudiwa.

Amesema, jumuiya ya kimataifa inatarajia kutimiza maendeleo yenye usawa, endelevu na usalama zaidi, na inapaswa kushika fursa, kukabiliana na changamoto, kuhimiza utekelezaji wa makubaliano ya maendeleo ya dunia, ili kutimiza siku za baadaye zenye amani na ustawi zaidi.