Xi Jinping na baba yake Xi Zhongxun
2022-06-19 13:17:55| cri

Watu wanasema rais Xi anafanana sana na baba yake Xi Zhongxun katika uhusiano karibu na umma. Wao wote ni Wakomunisti wenye nia thabiti ya kuwahudumia wananchi.

Rais Xi pia amerithi moyo mzuri kutoka baba yake. Mwaka 1978, Xi Zhongxun aliyekuwa na umri wa miaka 65 aliteuliwa kuwa mkuu wa mkoa wa Guangdong. Aliwahi kukagua wilaya 21 za mkoa huo kwa siku mfululizo katika majira ya joto, kwani alikuwa anzingatia sana uchunguzi katika ngazi ya shina. Rais Xi pia amefanya hivyo. Tangu awe rais wa China, amefanya ukaguzi katika maeneo mbalimbali nchini China hata baadhi ya sehemu ziko mbali sana milimani.
Wakati huo, Rais Xi Jinping ambaye alikuwa anasoma katika chuo kikuu cha Qinghua alikwenda pamoja na baba yake kufanya ziara ya ukaguzi mkoani Guangdong, wakati akiwa kwenye mapumziko ya majira ya joto.
Rais Xi Jinping alimtazama baba yake, na kukumbuka wajibu wake moyoni wa kuwahudumia wananchi na kulistaiwsha taifa la China.
Rais Xi pia amerithi desturi ya kubana matumizi kutoka baba yake. Anapofanya ukaguzi, huwaagiza wafanyakazi wake kuhesabu vizuri matumizi ya safari, hata baadhi ya wakati analala kwenye treni.
Upendo wa baba wa Xi Jinping umekuwa mkubwa, Bw. Xi Zhongxun aliwekaf mfano wa kuigwa na kurithisha desturi ya familia.
Bw. Xi Zhongxun alikuwa mfanyakazi mwanamapinduzi hodari, ambaye amemrandisha sana mtoto wake Xi Jinping. Wote wana moyo wa kukubali wajibu, na wanaonyesha mfano wa kuigwa kwa kauli na vitendo, na kuwahudumia wananchi kwa moyo wote.
Kwenye barua yake kwa baba, rais Xi Jinping alisema, wewe ni kama mtumishi unayefanya kazi kazi kwa bidii kwa ajili ya watu wa China. Hii pia inanihamasisha kuchangia maisha yangu yote katika mambo ya kuhudumia wananchi.