Msanii maarufu wa China abuni kazi maalumu za sanaa kwa ajili ya Siku ya Akina Baba Duniani ​
2022-06-20 08:58:29| CRI

Msanii maarufu wa China Profesa Han Meilin amebuni kazi maalumu za sanaa, ambazo ni nguo ndogo za pamba yenye herufi na alama za kale zilizotengenezwa na udongo wa mfinyanzi, kwa ajili ya kusherehekea Siku ya Akina Baba Duniani, inayoangukia leo terehe 19 mwezi wa Juni.

Upendo wa baba huwa ni mchangamfu na wenye nguvu thabiti, na  wanachotarajia akina baba ni upendo wenye kujali kutoka kwa watoto wao, ambao ni kama nguo ya pamba inayoweza kuleta joto wakati wa baridi. Kazi hizo za udongo wa mfinyanzi zilizotengenezwa na Profesa Han Meilin pamoja na mwanafunzi wake Chao Ziwei zinamaanisha upendo huo mzito ambao pia unaweza kustahimili changamoto mbalimbali katika maisha yetu.

Profesa Han Meilin, mwenye umri wa miaka 86, amepata mafanikio makubwa katika sekta ya sanaa. Na herufi na alama za kale zilizotumika kwenye kazi hizo ni kati ya makumi ya maelfu ya herufi na alama za kale ambazo Profesa Han alizikusanya kwa juhudi kubwa kutoka maandishi kwenye mifupa, mawe, ufinyanzi na vifaa vingine mbalimbali vya kale vilivyobaki na ilimchukua miaka mingi kukusanya masalia haya ya kiutamaduni na kutunga kitabu cha “Tianshu".