Tunapaswa kulinda mazingira kama macho yetu, na kuyathamini kama maisha yetu
2022-06-20 14:10:30| CRI

Siku ya Mazingira Duniani huangukia Juni 5 kila mwaka. Rais Xi Jinping wa China amesisitiza kwamba “Tunapaswa kulinda mazingira kama macho yetu, na kuyathamini kama maisha yetu”. Katika miaka mitano iliyopita, Xi ambaye pia ni katibu mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) alitoa hotuba mbalimbali juu ya mada hii inayoonesha jinsi alivyobeba ipasavyo wajibu wa mkuu wa nchi kubwa kama China.