Rais Xi atoa wito wa kufanya juhudi za uratibu dhidi ya vitendo vya ufisadi
2022-06-20 09:23:02| CRI

Rais Xi Jinping wa China amesema kupambana na ufisadi ni suala muhimu zaidi la kisiasa ambalo linahusu imani na uungaji mkono wa watu, na kusisitiza kuwa hivi ni vita tusivyopaswa kushindwa.

Akiendesha semina ya 40 ya mafunzo ulioandaliwa na ofisi ya siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti na kujadili suala la kufanya juhudi za uratibu ili kuhakikisha maafisa hawathubutu, hawawezi wala hawatamani kufanya ufisadi, Xi Jinping ambaye pia ni Katibu Mkuu wa CPC, amesema maafisa wanapaswa kuelewa kwa kina uboreshaji wa maadili ya chama, kujenga serikali safi na kupambana na ufisadi chini ya mazingira mapya, na kuongeza uwezo wao wa kuboresha juhudi za uratibu ili kuhakikisha maafisa hawathubutu kufanya vitendo vya ufisadi na wala hawapati fursa au kutamani kufanya hivyo, kwa lengo la kuweza kushinda vita hivi vigumu na vya muda mrefu kwa pande zote.

Rais Xi amebainisha kuwa tangu mkutano mkuu wa 18 wa chama uliofanyika mwaka 2012, China imeshuhudia mafanikio makubwa katika kupambana na ufisadi na kujikusanyia uzoefu wenye thamani.