Raia 132 wauawa katikati mwa Mali
2022-06-21 09:51:27| CRI

Serikali ya Mali imetoa taarifa ikisema jumla ya raia 132 waliuawa katika vijiji vitatu huko Bankass katikati mwa Mali.

Mamlaka nchini Mali zimesema wakazi waishio kwa amani wa vijiji vya Diallassagou, Dianweli, Deguessagou na sehemu zilizo karibu na Bankass wamekuwa wahanga wa mashambulizi haya ya kikatili yaliyotokea usiku wa Juni 18 hadi 19.

Wahusika kadhaa wa mauaji hayo wametambuliwa rasmi, ambao ni sehemu ya wapiganaji wa kundi la Katiba Macina of Amadou Koufa

Serikali inalaani vikali mashambulizi hayo na kuahidi kutumia njia zote kuwatafuta wahusika na kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria.

Mali imekuwa ikikabiliwa na migogoro ya kiusalama, kisiasa na kiuchumi tangu mwaka 2012, huku uasi, uvamizi wa wanajihadi na ghasia baina ya jamii zikiua maelfu ya watu na wengine mamia ya maelfu kuwa wakimbizi nchini humo.