Mjumbe maalumu wa China atoa wito wa kuondoa vikwazo dhidi ya Sudan Kusini
2022-06-21 09:46:42| CRI

Naibu mjumbe wa kudumu wa China kwenye Umoja wa Mataifa Balozi Dai Bing, ametoa wito wa kuondolewa kwa vikwazo vilivyowekwa na Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa, na vikwazo vya upande mmoja vilivyowekwa na baadhi ya nchi dhidi ya Sudan Kusini.

Balozi Dai amesema kipindi cha mpito cha Sudan Kusini kitamalizika mwakani, pande zote husika za Sudan Kusini zinatarajiwa kudumisha kasi iliyopo sasa ya kusonga mbele kwa utulivu na utaratibu, ili kufikia malengo ya sasa ya mpango wa mpito wa kisiasa, na mipango ya usalama na mageuzi ya kiuchumi.

Kuhusu changamoto maalumu zinazoikabili Sudan Kusini katika kutekeleza makubaliano ya kurejesha amani, amesema jumuiya ya kimataifa inapaswa kuwa na uvumilivu na kuisaidia nchi hiyo kukabiliana na changamoto, badala ya kuendelea kuishinikiza, kuilaumu na kuiwekea vikwazo.