China yaipinga Marekani kutekeleza “Sheria ya kuzuia Wauyghur kufanyishwa kazi kwa nguvu”
2022-06-22 09:28:28| CRI

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Bw. Wang Wenbin jana alisema China inalaani vikali na kupinga kithabiti ile inayoitwa “Sheria ya kuzuia Wauyghur kufanyishwa kazi kwa nguvu” iliyotungwa na Marekani.

Wang amesema suala zima la “kufanyishwa kazi kwa nguvu huko Xinjiang” ni uwongo mkubwa uliotungwa na watu wanaoipinga China ili kuikashfu China, kitendo ambacho kinakwenda kinyume kabisa na haki ya wafanyakazi na maslahi ya watu wote wa makabila madogomadogo ya Mkoa unaojiendesha wa Kabila la Wauigur wa Xinjiang, China.

Amesema hiyo ni ishara tosha kwamba Marekani inataka kulazimisha kuwepo kwa hali ya watu kupoteza ajira mkoani Xinjiang kupitia njia za kisheria, na kuifanya China itengwe na dunia, kitendo ambacho kinaonyesha umwamba wa Marekani. China itachukua hatua zenye nguvu ili kulinda kithabiti haki halali ya makampuni na watu wa China.