Rais Xi Jinping ahutubia ufunguzi wa baraza la biashara la BRICS
2022-06-22 21:32:06| cri

Rais Xi jinping wa China leo ametoa hotuba muhimu kwenye ufunguzi wa baraza la biashara la nchi za BRICS lililofanyika kwa njia ya video.

Baraza la 14 la biashara la BRICS linatarajiwa kufanyika alhamisi kwa njia ya video, likiwa na kaulimbiu ya”kuendeleza ushirikiano wa hali ya juu wa BRICS, na kuleta zama mpya ya maendeleo ya dunia”.

Rais Xi Jinping pia amesema China itaendelea kufungua mlango na kuhimiza mazingira ya biashara kwa mujibu wa kanuni za soko, zinazoongozwa na sheria na kufuata vigezo vya kimataifa.

Ameyahimiza makampuni kuwekeza na kujiendeleza nchini China, kuhimiza biashara na ushirikiano wa kiuchumi, na kuchangia fursa za maendeleo.