China yatoa wito wa kuondolewa kwa vikwazo vya silaha kwa CAR
2022-06-23 09:12:30| CRI

Naibu mwakilishi wa kudumu wa China kwenye Umoja wa Mataifa balozi Dai Bing jana alitoa wito kwa Baraza la Usalama kuondoa vikwazo vya silaha nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati (CAR) haraka iwezekanavyo.

Waziri wa Mambo ya Nje wa CAR alimwandikia mwenyekiti wa Baraza la Usalama Juni 8, akieleza kwamba vikwazo vya silaha vina athari kubwa katika kudumisha usalama wa nchi hiyo, na kusisitiza juhudi kubwa za serikali ya CAR katika kutekeleza maazimio ya Baraza la Usalama na kuwezesha kuondolewa kwa vikwazo vya silaha.

Balozi Dai amesema China inatumai kuwa Baraza la Usalama litasikiliza ombi la CAR na kuondoa vikwazo mapema, ili kutoa msaada kwa CAR katika kushughulikia changamoto za kiusalama na kudumisha utulivu wa taifa. Alitoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kusaidia kukuza uchumi wa CAR na kuboresha hali ya kibinadamu.