Rais Xi asisitiza umuhimu wa kujenga mifumo ya msingi ya data na kuboresha usimamazi wa vitengo vya utawala
2022-06-23 09:10:00| CRI

Rais wa China Xi Jinping jana Jumatano alitoa wito wa kufanywa juhudi za kuharakisha ujenzi wa mifumo ya msingi ya data na kuboresha kazi katika vitengo vya utawala.

Akiwa kama mwenyekiti wa mkutano wa 26 wa tume ya kuimarisha mageuzi ya jumla ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China CPC, rais Xi ambaye pia ni katibu mkuu wa CPC amesisitiza umuhimu wa mifumo ya msingi ya data katika maendeleo na usalama wa taifa, na kutaka kufanywa juhudi zaidi za kulinda usalama wa data za taifa, kulinda taarifa binafsi na siri za biashara, na kuwezesha uchumi halisi uwe na mzunguko na matumizi sahihi zaidi ya data.

Mkutano huo uliangalia na kupitisha miongozo ya mifumo ya msingi ya data, pamoja na mipango ya kazi ya kufanya mageuzi ya majaribio ya tathmini ya watumishi wa sayansi na teknolojoia na kuimarisha usimamizi wa biashara za jukwaa kuu la malipo. Mkutano huo pia ulihudhuriwa na wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya CPC, wakiwemo Li Keqiang, Wang Huning na Han Zheng.