Rais Xi Jinping atoa hotuba muhimu kwenye hafla ya ufunguzi wa Baraza la Biashara la BRICS
2022-06-23 09:12:02| CRI

Rais wa China Xi Jinping amehudhuria hafla ya ufunguzi wa Baraza la Biashara la BRICS iliyofanyika kwa njia ya mtandao wa internet na kutoa hotuba muhimu yenye kichwa kisemacho “Fuatilia Mwenendo wa Nyakati ili Kujenga Mustakabali Mzuri”.

Kwenye hotuba yake rais Xi amesema hivi sasa dunia inakabiliwa na mabadiliko makubwa pamoja na janga ambayo hayajawahi kushuhudiwa katika karne nzima iliyopita. Changamoto mbalimbali za kiusalama zinaendelea kuibuka. Uchumi wa dunia bado unakabiliwa na dhoruba kali ukiwa njiani kuelekea kufufuka, na maendeleo ya dunia yamepata vizuizi vikubwa. Hivyo rais Xi ameshauri kwanza, kushikamana na kufanya uratibu na kudumisha kwa pamoja amani na utulivu duniani. Pili, kuwasiliana na kuhimiza maendeleo endelevu ya dunia, kwani maendeleo ndio ufunguo wa kutatua matatizo mbalimbali magumu na kuwapa watu maisha mazuri. Tatu kushirikina pamoja kwenye mambo magumu na kutafuta ushirikiano wa kunufaishana. Na nne kuwa na ujumuishi na kuongeza uwazi na mafungamano.

Aidha amesema China itaendelea kuinua kiwango cha juu cha kufungua mlango, kukuza mifumo mipya ya uchumi ulio wazi wa viwango vya juu na kuendelea kuhimiza soko lenye msingi wa sheria na kufanya mazingira ya biashara yawe ya kimataifa. Amesema ushirikiano wa BRICS sasa umeinigia kwenye hatua mpya ya maendeleo yenye ubora zaidi.