Kenya yaanzisha kampeni ya kuhamasisha soko la utalii wa ndani
2022-06-24 09:08:20| CRI

Bodi ya Utalii ya Kenya (KTB) jana ilizindua kampeni ya kuhamasisha soko la utalii wa ndani ili kuchochea sekta ya utalii inayoendelea kufufuka kutokana na janga la COVID-19.

Bodi hiyo imesema kampeni hiyo inawahamasisha watu wa Kenya kutembelea maeneo mbalimbali ya utalii nchini humo ili kuiunga mkono sekta ya utalii ya Kenya, na kulifanya soko la ndani liwe nguzo muhimu ya sekta hiyo inayoathiriwa vibaya na janga la Corona.

Mkurugenzi mtendaji wa bodi ya KTB Bibi Betty Radier alitoa taarifa mjini Nairobi akisema KTB imefanya ushirikiano na sekta ya biashara ya usafiri nchini ili kuifanya kampeni hiyo iwe na ushawishi, kupitia kutoa ya seli vifurushi vya utalii. Amesema washirika wao wa biashara ya usafiri wataunganisha rasilimali, habari na soko ili kudumisha mahitaji ya muda mrefu kwenye sekta ya utalii ya ndani.