Wall Street yawa na wasiwasi zaidi na uwezekano wa mdororo wa uchumi wa Marekani mwakani
2022-06-24 09:05:02| CRI

Wachumi kutoka makampuni makubwa ya Wall Street yakiwemo Goldman Sachs na Morgan Stanley wametabiri uwezekano mkubwa wa kudorora kwa uchumi wa Marekani katika mwaka ujao.

Shirika la Reuters lilitoa ripoti likisema, "Goldman Sachs inatabiri kwamba kuna uwezekano wa asilimia 30 kwa uchumi wa Marekani kudorora katika mwaka ujao, ambayo ni kutoka asilimia 15 ya hapo awali, kufuatia mfumuko mkubwa wa bei katika historia ya nchi hiyo na hali duni ya uchumi mkuu kutokana na mzozo wa Ukraine.

Wachumi kutoka Morgan Stanley Jumanne pia walionesha kuwepo uwezekano wa kushuka kwa uchumi katika miezi 12 ijayo kwa karibu asilimia 35.