Siku ya kimataifa ya Wajane
2022-06-24 10:38:53| CRI

    Tarehe 23 Juni ya kila mwaka ni Siku ya Kimataifa ya Wajane. Siku hii imeanza kuadhimishwa mwaka 2011 na Umoja wa Mataifa, lengo kuu likiwa ni kusikilizwa kwa sauti na mambo wanayopitia wajane na kuwaunga mkono pale wanapohitaji. siku hii pia inatumika kama fursa ya kuchukua hatua ya kutimiza kikamilifu haki na kuwatambua wajane, ikiwa ni pamoja na kuwapa taarifa muhimu zinazohusiana na haki ya urithi, haki ya kumiliki ardhi na rasilimali nyingine za uzalishaji, kazi nzuri na malipo sasa, lakini pia kuwapa fursa ya kupata mafunzo na elimu, kwa kuwa baadhi ya wajane wana umri mdogo na wana uwezo wa kuendelea na elimu. 

    Katika kipindi cha Ukumbi wa Wanawake cha wiki hii, tunaangalia madhila yanayowakabili wajane pindi waume zao wanapofariki.