Rais wa Zimbabwe awasifu wawekezaji wa China
2022-06-24 09:06:39| CRI

Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa amesifu makampuni ya China kwa uwekezaji wao nchini humo. Rais Mnangagwa amesema hayo baada ya kutembelea makao makuu ya Kampuni ya Saruji ya Sino-Zimbabwe mjini Gweru, akiisifu kampuni hiyo kupanua shughuli zake nchini Zimbabwe.

Kampuni ya Sino-Zimbabwe, ambayo sasa inafanya kazi kwa asilimia 90 katika matumizi ya uwezo wake, ni kampuni ya tatu kwa uzalishaji mkubwa wa saruji nchini Zimbabwe.

Rais Mnangagwa amesema kuwa uwekezaji wao haupo tu katika utengenezaji wa saruji, bali pia katika kutengeza matofali tofauti yenye ubora wa juu.

Aliitaka kampuni hiyo kuendelea kutumia fursa ya soko lililoshamiri katika sekta ya ujenzi nchini Zimbabwe ili kukuza biashara yake.

Ameongeza kuwa uchumi wa Zimbabwe umebadilika kutoka hali ya utulivu hadi ukuaji na serikali itaendelea kuwavutia wawekezaji wengine ili kuhimiza ukuaji wa uchumi. Amesema shughuli za uchumi zinaendelea kukua, ikiwemo shughuli za viwanda, ambapo uwezo wa uzalishaji unaendelea kukua na kufikia asilimia 75.