Vijana wa Afrika watoa mwito wa kuwekwa ajenda ya uhifadhi wa viumbeanuai inayozingatia binadamu
2022-06-24 09:07:39| CRI

Wanaharakati vijana jana walisema kuwa, jamii za mashinani barani Afrika zinapaswa kuwa kiini cha mazungumzo ya dunia kwa ajili ya kufikia makubaliano muhimu kuhusu k kulinda mazingira ya asili katika miongo kadhaa ijayo.

Mwakilishi wa Mtandao wa Vijana wa Uhifadhi Viumbeanuai Duniani tawi la Uganda Derrick Mugisha amesema kuwa, njia zinazotoa kipaumbele kwa  binadamu ili kuimarisha uhifadhi wa mfumo muhimu wa kiikolojia zinahitajika barani Afrika, ambapo hali ya kupoteza mazingira ya asili  imesababisha umaskini, njaa na magonjwa kwa binadamu.

Mugisha aliyasema hayo alipohudhuria mkutano wa 4 wa kundi la kikazi wa mfumo wa viumbeanuai duniani baada ya mwaka 2020. Amesema kuwa, mchango wa jamii za wenyeji utakuwa muhimu ili kufikia makubliano shirikishi ya kurudisha  uhifadhi wa spishi.

Makundi yanayoongozwa na vijana yamependekeza kujumuisha matarajio ya jamii za wenyeji kwenye mswada wa mfumo wa viumbeanuai duniani baada ya mwaka 2020, mfumo huo unatarajiwa kupitishwa Jumapili hii mjini Nairobi.