Rais wa Afrika Kusini aomboleza vifo vya vijana 22 waliofariki kwenye ukumbi wa muziki
2022-06-27 08:37:02| CRI

Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa ameomboleza vifo vya vijana 22 waliofariki ndani ya ukumbi wa muziki katika eneo la East London, jimbo la Cap Mashariki alfajiri ya jana.

Taarifa iliyotolewa na Ikulu ya nchi hiyo imesema, rais Ramaphosa ameeleza wasiwasi wake juu ya ripoti za mazingira ya vifo hivyo, ambapo vijana wadogo walikusanyika katika eneo ambalo kisheria haliruhusu watu walio na umri wa chini ya miaka 18 kuingia. Taarifa hiyo haikueleza sababu ya tukio hilo, na kusema rais Ramaphosa anasubiri taarifa zaidi.

Polisi nchini Afrika Kusini wanaendelea na uchunguzi wa tukio hilo ambalo chanzo chake bado hakijajulikana.