Kenya yafanya shindano la ujuzi wa lugha ya Kichina
2022-06-27 08:47:37| cri


 

Chuo Kikuu cha Nairobi Ijumaa iliyopita kilifanya duru ya kwanza ya shindano la ujuzi wa lugha ya Kichina kwa wanafunzi wa vyuo vya kigeni.

Wanafunzi 15 wa vyuo vya Confucius kutoka vyuo vikuu vinne vya nchini Kenya walishiriki katika shindano hilo, ambapo waliwavutia waamuzi kwa ustadi wao wa kuzungumza lugha ya kichina, muziki wa kitamaduni, dansi na sanaa ya kung fu.

Naibu chansela wa Chuo Kikuu cha Nairobi, Stephen Kiama amesema, lugha ya Kichina imepata umaarufu miongoni mwa vijana wa Kenya na inatoa nafasi zaidi za kazi.

Hansnick Omondi Otieno kutoka Chuo cha Confucius katika Chuo Kikuu cha Nairobi alishinda tuzo ya kwanza na ataingia kwenye raundi inayofuata.