China kuongeza uwekezaji katika uhifadhi wa mazingira
2022-06-27 08:45:14| CRI

Wizara ya Mazingira ya China imehimiza kuongeza uwekezaji katika uhifadhi wa mazingira ya ikolojia wakati ikiendelea kufanya juhudi za kuleta utulivu wa uchumi.

Ikilenga miradi 102 ya ikolojia iliyoorodheshwa kati ya miradi mikubwa  ya nchi katika kipindi cha Mpango wa 14 wa Miaka Mitano wa Maendeleo (2021-2025), Wizara hiyo imesisitiza haja ya kuharakisha maendeleo ya miradi inayohusiana na hewa, maji, udongo, udhibiti wa uchafuzi wa taka ngumu za nyuklia, na usimamizi wa usalama wa mionzi.