Barabara ya mwendokasi ya Nairobi iliyojengwa na Kampuni ya China yapendekezwa kwenye tuzo ya miundombinu ya uchukuzi
2022-06-28 08:46:40| CRI

Taarifa iliyotolewa na Kampuni ya Moja Express inayosimamia barabara mpya ya Nairobi Expressway iliyojengwa na kampuni ya China nchini Kenya imesema, barabara hiyo imependekezwa katika kipengele cha ‘tuzo ya mwaka ya miundombinu ya uchukuzi’ katika uzinduzi wa Tuzo za Afrika Mashariki.

Hatua hiyo inakuja wiki chache baada ya barabara hiyo kuanza kufanya kazi kwa majaribio kabla ya kuzinduliwa rasmi. Matumizi yake yametoa fura mpya kwa wamiliki wa mabasi nchini Kenya, ambao wameanzisha njia mpya za safari, huku wamiliki wa magari wakifurahia muda mfupi wa safari.

Tuzo za Uchukuzi za Afrika Masharini ni za kwanza za aina yake katika kanda ya Afrika Mashariki, na zinalenga kusherehekea ufanisi wa sekta ya uchukuzi.