FAO yataka dola milioni 172 ili kuepusha janga la kibinadamu katika Pembe ya Afrika
2022-06-28 08:52:44| CRI

Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) limetaka msaada wa dola milioni 172 za kimarekani ili kusaidia kuepusha janga la kibinadamu katika eneo la Pembe ya Afrika.

Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari, FAO imesema dola milioni 219 za kimarekani zinahitajika ili kuzuia hali mbaya ya usalama wa chakula katika eneo hilo, lakini hadi sasa ni dola milioni 47 tu ambazo zimepatikana.

Katika taarifa hiyo, FAO imehimiza ufuatiliaji zaidi kwa nchi nne zinazoathiriwa zaidi na ukame, ambazo ni Djibouti, Ethiopia, Kenya na Somalia, na kutaka fedha ili kukidhi mahitaji ya kibinadamu ya karibu watu milioni tano vijijini katika nchi hizo.