China yakaribisha mipango yote ya kuhimiza ujenzi wa miundombinu duniani
2022-06-28 08:52:01| cri

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Bw. Zhao Lijian amesema, China daima inakaribisha mipango yote ya kuhimiza miundombinu duniani, na hakuna tatizo kuwa mipango husika mbalimbali inaweza kuchukua nafasi ya kila mmoja.

Zhao amesema hayo alipojibu swali kuhusu mpango mpya wa ujenzi wa miundombinu uliotolewa katika mkutano wa Kundi la Nchi 7 (G7). Hata hivyo amesema, China inapinga maneno na vitendo vinavyochafua na kukashifu Pendekezo la “Ukanda Mmoja, Njia Moja”, na kuendeleza hesabu za kijiografia na kisiasa kwa kisingizio cha ujenzi wa miundombinu.

Hivi karibuni, Rais wa Marekani Joe Biden alitangaza uzinduzi rasmi wa mpango wa "Ujenzi wa Miundombinu Duniani na Uhusiano wa Kiwenzi wa Uwekezaji" kwenye mkutano wa kilele wa Kundi la Nchi 7 (G7). Ofisa mmoja mwandamizi wa Marekani ambaye jina lake halijatajwa alidai kuwa, mpango huo mpya wa G7 utatoa njia mbadala kwa ushirikiano wa miundombinu unaosababisha "mtego wa madeni".