Kilimo cha mpunga wa kichina chapata mafanikio nchini Botswana
2022-06-29 09:09:46| CRI

Siku ya mavuno ya mpunga wa kichina imefanyika nchini Botswana ili kusherehekea mafanikio ya matumizi ya mbegu za mpunga wa kichina zinazostahimili ukame nchini Botswana.

Viongozi mbalimbali walishiriki kwenye siku hiyo, akiwemo makamu wa rais wa Botswana Slumber Tsogwane na balozi wa China nchini humo Wang Xuefeng.

Tsogwane amesema mafanikio ya upandaji wa mpunga wa kichina yana umuhimu mkubwa kwa Botswana katika kuongeza utoaji wa nafaka, kupunguza uagizaji wa chakula kutoka nje, na kuhakikisha usalama wa chakula. Ameongeza kuwa China ina teknolojia ya juu na uzoefu mkubwa katika uzalishaji wa kilimo, na anatarajia nchi hizo mbili zitaimarisha zaidi ushirikiano katika sekta ya kilimo.

Kwa upande wake, Balozi Wang amesema, China itaendelea kuimarisha ushirikiano wa kilimo na Botswana, na kuisaidia nchi hiyo kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi na kuboresha usalama wa chakula.