Rais Xi asisitiza kujitegemea katika sayansi na teknolojia ni msingi wa ustawi wa taifa
2022-06-29 15:07:36| CRI

Rais Xi Jinping wa China jana Jumanne alipofanya ziara ya ukaguzi katika mji wa Wuhan mkoani Hubei, katikati ya China, alisisitiza umuhimu wa kujitegemea kwenye sekta ya sayansi na teknolojia na kutaja kuwa ni msingi wa ustawi na usalama wa taifa.

Rais Xi ametaka dhana mpya ya maendeleo itekelezwe kikamilifu, kwa usahihi na kwa pande zote, na mkakati wa maendeleo yanayochochewa na mavumbuzi utekelezwe kwa kina, ili China ipige hatua kubwa zaidi kwenye njia ya kuendeleza sayansi na teknolojia kwa kujitegemea,  kuendelea kuimarisha usalama wa maendeleo ya nchi, kuendelea kuvumbua teknolojia mpya za hali ya juu na sekta mpya, kufungua nyanja mpya kwenye maendeleo ya uchumi, na kuongeza zaidi nguvu ya China kwenye ushindani wa kimataifa.