Idadi ya vifo vya wahamiaji waliokutwa ndani ya lori nchini Marekani yafikia 50
2022-06-29 08:39:28| CRI

Idadi ya wahamiaji waliokutwa wamefariki ndani ya lori lililotelekezwa mjini San Antonio, jimbo la Texas nchini Marekani imeongezeka na kufikia 50.

Radio ya Umma ya Texas ilimnukuu waziri wa mambo ya nje wa Mexico Marcelo Ebrard akisema kuwa, watu 46 walikutwa wamekufa katika eneo la tukio na wengine wanne walifariki wakiwa wanapata matibabu hospitali. Amesema kati ya marehemu hao, 22 ni raia wa Mexico, 7 wanatokea Guatemala, wawili wanatokea Hondura, na miili mingine 19 bado haijatambuliwa.

Maofisa wa huko wanasema, watu 16, wakiwemo watoto wanne, wamepelekwa hospitali kupata matibabu kutokana na uchovu unaotokana na joto kali na kukosa maji mwilini.

Habari zinasema, karibu watu 100 walikuwa ndani ya lori hilo.