Benki ya Maendeleo ya Afrika kuondoa matishio ya uwekezaji barani humo ili kukuza maendeleo ya kijani
2022-06-29 08:38:30| CRI

Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) imesema kuwa itaondoa tishio la mabadiliko ya tabianchi katika uwekezaji barani Afrika ili kukuza ukuaji wa kijani katika bara hilo.

Mratibu mkuu wa mipango katika Idara ya Mabadiliko ya Tabianchi na Ukuaji wa Kijani katika Benki hiyo Bi. Daninah Milenge-Uwella amesema hayo katika Mkutano wa 48 wa Jumuiya ya Bima Afrika uliofanyika mjini Nairobi, Kenya. Amesema Benki hiyo itachukua hatua mbalimbali ikiwemo udhamini wa mikopo na msaada wa kiufundi ili kupanua udhamini wa kijani.

Amesema lengo kuu ni kuwashawishi na kuwavutia wawekezaji wa sekta binafsi kuwekeza katika maeneo ya hatari zaidi kama teknolojia zinazolinda mazingira, na kuongeza kuwa, Benki hiyo ina nia ya kuunganisha ukuaji wa uchumi na tatizo la utoaji wa hewa chafu barani Afrika.