Kiongozi wa Sudan asisitiza haja ya uhusiano wa kawaida na usawa na Ethiopia
2022-06-29 08:37:36| CRI

Mwenyekiti wa Baraza la Utawala wa Mpito nchini Sudan Abdel Fattah Al-Burhan amerejea tena nia thabiti ya nchi hiyo ya kuwa na uhusiano wa kawaida na usawa na Ethiopia.

Taarifa iliyotolewa na Baraza hilo imesema, Al-Burhan amesema hayo alipokutana na Mjumbe Maalum wa Umoja wa Ulaya kuhusu masuala ya Pembe ya Afrika, Annette Weber, ambaye yuko ziarani nchini Sudan.

Viongozi hao walijadili mvutano katika eneo la Fashaga kwenye mpaka wa Sudan na Ethiopia na mauaji ya askari saba na raia wa Sudan yaliyofanywa na jeshi la Ethiopia.