Kiongozi wa Sudan asema jeshi linatarajia kukabidhi madaraka kwa serikali itakayochaguliwa
2022-06-30 08:48:56| CRI

Mwenyekiti wa Baraza la Utawala la Mpito la Sudan Abdel Fattah Al-Burhan amesema, vikosi vya jeshi la Sudan vinatarajia serikali itakayochaguliwa kubeba jukumu la kuitawala nchi.

Taarifa iliyotolewa jana na Baraza hilo imesema, wakati akikagua vikosi maalumu vya kijeshi huko Khartoum, Al-Burhan alisema njia pekee ya kutimiza hilo ni ama kufikia maafikiano ya kina ya kitaifa au uchaguzi, lakini si kwa maandamano au hujuma.

Kiongozi huyo alitoa wito wa kutumia haki ya kujieleza kupitia maandamano ya amani ambayo yanalinda mali za umma na za binafsi na hayadhuru maslahi ya raia wengine.

Maandamano makubwa ya kudai utawala wa kiraia yanatarajiwa kufanyika mjini Khartoum na miji mingine nchini Sudan hii leo.