Rais Xi Jinping wa China akutana na Ofisa Mkuu wa Mkoa wa Utawala Maaluma wa Hong Kong Bibi Carrie Lam
2022-06-30 20:43:11| CRI

Rais Xi Jinping wa China amekutana na Ofisa Mkuu wa Mkoa wa Utawala Maaluma wa Hong Kong Bibi Carrie Lam Alhamisi huko Hong Kong, China. Rais Xi amesema kuwa serikali ya China inatambua kikamilifu kazi nzuri aliyofanya Bibi Carrie Lam katika kipindi cha miaka mitano iliyopita tangu alipochukua wadhifa huo. Rais Xi anatarajia Bibi Carrie Lam kuunga mkono ofisa mkuu mpya na serikali ya awamu mpya ya Hong Kong katika juhudi zao za kutawala mkoa huo kwa mujibu wa sheria na kuendelea kutoa mchango kwa maendeleo ya Hong Kong na taifa la China.