Umoja wa Afrika watoa wito wa kujizuia na kufanya majadiliano kutatua mvutano kati ya Ethiopia na Sudan
2022-06-30 08:43:16| CRI

Mwenyekiti wa Kamati ya Umoja wa Afrika (AU) Moussa Faki Mahamat ametoa wito kwa Ethiopia na Sudan kujizuia na kuanzisha majadiliano kuhusu mgogoro katika mpaka kati ya  nchi hizo mbili.

Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari, Mahamat amesema, anafuatilia kwa makini mvutano wa kijeshi unaozidi kuwa mbaya kati ya Ethiopia na Sudan, na anasikitishwa na vifo vya watu vilivyotokea katika mpaka kati ya  nchi hizo.

Amezitaka nchi hizo mbili kuendelea kutoa mchango katika suluhisho la amani la mgogoro huo chini ya Mpango wa Mpaka wa Umoja wa Afrika, huku akitoa wito kwa nchi hizo mbili wanachama wa Umoja huo kumaliza migogoro kwa ajili ya maslahi ya utulivu wa kikanda na usalama wa pamoja.

Ethiopia na Sudan zinalaumiana kwa uchochezi kufuatia tukio lililotokea kwenye mpaka kati ya nchi hizo mbili wiki iliyopita.