Rais Xi Jinping asema mustakbali wa Hong Kong utakuwa mzuri zaidi kama sera ya "nchi moja, mifumo miwili" inaendelea kutekelezwa kithabiti
2022-06-30 19:09:00| CRI

Rais Xi Jinping wa China amewasili mkoani Hong Kong leo Alhamisi ambapo yeye na mkewe Bibi Peng Liyuan wamekaribishwa na watu wa Hong Kong kwenye kituo cha treni cha Kowloon Magharibi.

Akihutubia katika hafla ya kumkaribisha iliyofanyika kwenye kituo hicho, Rais Xi amesema siku zote anafuatilia hali ya Hong Kong na kila wakati yeye na serikali ya China wanasimama kithabiti na ndugu wa Hong Kong. Amesema Hong Kong imeonyesha nguvu kubwa ya uhai  baada ya kushinda changamoto mbalimbali katika muda uliopita. Uzoefu umethibitisha kwamba sera ya "nchi moja, mifumo miwili" ni sera inayofaa katika kuhakikisha ustawi na utulivu wa kudumu wa Hong Kong na kulinda maslahi ya ndugu wa Hong Kong. Rais Xi pia amesema Hong Kong hakika itakuwa na mustakabali mzuri zaidi na kutoa mchango mpya na mkubwa zaidi katika kutimiza ustawi mpya wa taifa la China, kama sera hiyo itaendelea kutekelezwa kithabiti.

Julai Mosi Rais Xi Jinping atahudhuria mkutano wa kuadhimisha miaka 25 tangu Hong Kong irudi China, sherehe ya kuapishwa kwa serikali ya awamu ya sita ya mkoa wa Hong Kong, na pia anatarajiwa kufanya ziara za ukaguzi kwenye sehemu mbalimbali za mkoa huo.