China yasema hatua za kimataifa za usalama barabarani hazipaswi kuziacha nyuma nchi zinazoendelea
2022-07-01 08:37:44| cri

Mjumbe wa kudumu wa China katika Umoja wa Mataifa Balozi Zhang Jun amesema, nchi zinazoendelea zinahitaji kuungwa mkono zaidi na jumuiya ya kimataifa katika sekta ya miundombinu ya usafiri wa barabarani, na utekelezaji wa hatua husika za usalama barabarani unapaswa kutoziacha nyuma nchi hizo.

Balozi Zhang pia amesema, usalama barabarani ni sehemu muhimu ya kutimiza maendeleo endelevu, na kuongeza kuwa, takwimu zinaonyesha kuwa 90% ya majeruhi duniani kutokana na ajali za barabarani kila mwaka wanatokea katika nchi zinazoendelea.